MCHEZAJI wa timu ya mpira wa mikono ya Kanda ya Unguja, Yussuf Abdalla (katikati) akichuana na wachezaji wa mkoa wa Mara kwenye uwanja wa Butimba, Mwanza. Timu hizo zilitoka sare 11-11. (PICHA NA AMEIR KHALID)

Yaanza kutwaa medali tatu

NA AMEIR KHALID, MWANZA
TIMU za Zanzibar zitashuka dimbani leo asubuhi kucheza hatua ya robo na fainali ya mashindano ya Umisseta, katika viwanja vya Butimba, Mwanza.

Katika michezo hiyo, Kanda ya Unguja itacheza fainali ya mpira wa meza kwa wanaume na wanawake ambapo mchezaji, Sultani Suleiman atacheza dhidi ya mkoa wa Dar es Salaam wakati fainali nyengine itachezwa upande wa wanawake kupitia kwa Mwanajuma Bakari wa mkoa wa Mwanza.

Kanda ya Unguja ilifikia hatua ya fainali baada ya kushinda katika michezo ya nusu fainali ambapo Sultani alishindi seti 2-0 dhidi ya Kilimanjaro, wakati Mwanajuma alishinda seti 2-0 mbele ya mkoa wa Manyara.

Katika mchezo wa riadha, Kanda ya Unguja ilianza kupata medali baada ya mkimbiaji wake, Mohamed Rashid kushika nafasi ya pili mita 100 na kutwaa medali ya fedha sawa na Nasra Abdalla aliyeshinda mbio za mita 100 wanakwe. Mwanariadha Omar Rashid alipata medali ya shaba kwa kushika nafasi ya tatu.

Pia michezo mengine ya robo fainali itachezwa kwa upande wa mpira wa mkono ambapo itacheza na mshindi wa pili wa kundi ‘C’ huku Kanda ya Pemba upande wa soka ikicheza robo fainali. Pemba imeongoza kundi lake la ‘B’ baada ya kutoka sare ya 1-1 dhidi ya Simiyu, bao lake likifungwa na Mohamed Abrhamani.

MAONI YAKO