NA ZAINAB ATUPAE
LIGI Kuu ya Zanzibar hatua ya nane bora inatarajiwa kuanza baada ya michuano ya Kombe la Kagame inayotarajiwa kuanza kutimua vumbi Juni 29 jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na Zanzibar Leo, Katibu Mkuu wa Chama cha Soka Zanzibar (ZFA),Mohamed Ali Hilali ‘Tedy’, amesema, wamelazimika kufanya hivyo kwa ajili ya kuipa nafasi JKU kushiriki vyema mashindano hayo.

Aidha, alisema, kufanya hivyo kutawawezesha kucheza ligi hiyo bila ya kuwepo viporo kutokana na kutokuwepo kwa JKU ambayo ni miongoni mwa klabu nane zilizofuzu hatua hiyo.

Alisema Ligi Kuu ya Zanzibar itaendelea kuitumikia kanuni ile ya mwaka huu mpaka msimu ujao ambao kanuni mpya zitaanza rasmi.

Mbali na JKU, miamba mengine kwenye ligi hiyo ni Zimamoto, KVZ na Mafunzo kwa upande wa Unguja.
Kwa upande wa Pemba ni pamoja na wakongwe Jamhuri, Mwenge, Opec na Hardrock.

MAONI YAKO