MABADILIKO ya hali ya hewa duniani yanayotokana na ongezeko la joto yamepewa jina la tabianchi, tatizo ambalo limekuwa na athari kubwa zinazoendelea kushuhudiwa kila kukicha.

Tafiti mbalimbali zilizofanywa duniani zinaeleza kuwa nchi zenye maendeleo ya viwanda ndizo zinazoongoza kwa uzalishaji wa gesi zinazoongeza joto la dunia.

Athari zake hivi sasa ni kuongezeko la joto ambalo limekuwa likiyeyusha theluji hali inayochangia kuongezeka kwa kina cha maji ya bahari kiasi cha kuvifunika baadhi ya visiwa vigogo vidogo hapa ulimwenguni.

Athari za tabia nchi zimeanza kuvifikia kwa uwazi visiwa vya Zanzibar kwani katika baadhi ya maeneo ambayo wazee wetu walikuwa wakilima yameingiliwa na maji ya bahari.

Aidha athari za tabia nchi zimekuwa zikibadilisha miongo kwani misimu ya mvua hasa hapa nchini kwetu Zanzibar kwa jumla, imebadilika na kuathiri shughuli za kilimo na kupunguza uzalishaji.

MAONI YAKO