ROME, Italia

MENEJA wa zamani wa Manchester City, Roberto Mancini,ametajwa kama meneja mpya wa timu ya taifa ya Italia.

Kocha huyo mwenye umri wa miaka 53,amekubali mkataba wa miaka miwili akirithi mikoba ya Gian Piero Ventura ambaye alitupiwa virago baada ya Italia kushindwa kufuzu fainali za Kombe la Dunia nchini Russia.

Itakuwa jukumu la kwanza la kimataifa la Mancini, ambaye aliondoka katika klabu ya Russia ya Zenit St Petersburg kwa jili ya kuchukuwa nafasi hiyo.

Aliiongoza Manchester City kutwaa taji kwa mara ya kwanza baada ya miaka 44 mwaka 2012.

Tokea kuondoka kwenye dimba la Etihad mwaka 2013, Mancini aliifundisha  Galatasaray na Inter Milan kabla ya kujiunga na Zenit mwezi Juni mwaka 2017.(BBC Sports).

MAONI YAKO