LONDON, England

MENEJA wa Arsenal Arsene Wenger, amezungumza kuhusu kuwaenzi wachezaji kutoka Afrika wakati wa mkutano wake wa mwisho kama meneja ya klabu hiyo.

Kwenye mkutano huo, Wenger, alisema, wachezaji kutoka Afrika walikuwa wenye mchango mkubwa katika taaluma yake akiwa meneja wa soka England.

“Nilikuwa na wachezaji wa Afrika maisha yangu yote. Nilifungua skuli na moja wa marafiki zangu. Watu kama Yaya Toure, Kolo Toure, Emmanuel Eboue, Gervinho walikuja nami kutoka skulini”, alisema Wenger.

Rais wa sasa wa Liberia, George Weah ni kati ya wachezaji kutoka Afrika aliowakuza Wenger.

“Nilkuwa na George Weah tangu akiwa na umri mdogo sana na Youssou Fofana kutoka Ivory Coast. Nilikuwa na Lauren Etame Maye kutoka Cameroon. Kawaida nilikuwa na wachezaji wa Afrika kwenye kikosi changu. Walikuwa wenye mchango mkubwa.”

Wenger aliongoza mechi ya mwisho ya Arsenal juzi Jumapili dhidi ya Huddersfield kwenye uwanja wa John Smith. Kikosi chake kiliibuka na ushindi bao 1-0.

Wenger anaondoka Arsenal baada ya kusimamia mechi 1,235 ambapo alipata ushindi michezo 716 na magoli 2,298. Arsenal bado hawajamteua mrithi wake.

Alex Iwobi na Pierre-Emerick Aubameyang ni miongoni mwa wachezaji wa hadhi ya juu kwa sasa hapo Arsenal.

Kuanzia rais wa sasa wa Liberia, Weah huko Monaco hadi mchezaji wa mwisho aliyesaini raia wa Gabon, Pierre-Emerick Aubameyang, Wenger amekuwa mtu muhumu kwa wachezaji wa Afrika.

Kuwasaini na kuwakuza wachezaji bora zaidi wa Afrika ni kitu ambacho Wenger amekifanya katika miaka yake yote 22 akiwa na Arsenal.

Jumla ya wachezaji 16 kutoka Afrika waliichezea Arsenal chini ya usimamizi wa Wenger.
Jeshi la Wenger kutoka Afrika ni pamoja na Emmanuel Adebayor (Togo)
Alex Iwobi (Nigeria), Pierre-Emerick Aubameyang (Gabon), Nwankwo Kanu (Nigeria)
Marouane Chamakh (Morocco), Lauren Maye (Cameroun) na Kaba Diawara (Guinea).

Wengine ni Quincy James Owusu (Ghana), Emmanuel Eboue (Ivory Coast), Alex Song (Cameroun), Mohamed Elneny (Misri), Kolo Toure (Ivory Coast), Emmanuel Frimpong (Ghana), Armand Traore (Senegal), Gervinho (Ivory Coast) na Christopher Wreh.

NWANKO KANU

Mshindi mara mbili wa tuzo la mchezaji bora Afrika, Nwankwo Kanu ni mmoja wachezaji bora zaidi kutoka Afrika kuwahi kufanya kazi chini ya Wenger, Arsenal.
Akiwa na Arsenal, Mnigeria huyo alishinda mataji mawili ya Ligi Kuu ya England, Kombe la FA na pia Community Shield.

Baada ya kujiunga na Arsenal mwaka 1999, Kanu alifunga magoli 44 kwenye mechi 198 alizocheza kabla ya kuhamia West Bromwich Albion mwaka 2004.
Anakumbukwa sana kwa ‘hat-trick’ yake ya pili dhidi ya Chelsea.

LAUREN ETAME MAYE

Raia wa Cameroun, Lauren Maye alifunga mabao 9 kwenye mechi 241 alizocheza, lakini, kawaida alikuwa ni mchezaji aliyekuwa anategemegwa sana.

Alisainiwa na Wenger mwaka 2000 kama winga na kuibuka kuwa mmoja wa wachezaji bora zaidi wa safu ya nyuma katika Ligi Kuu ya England na hasa Arsenal hadi alipoondoka na kuelekea Portsmouth mwaka 2007.

Lauren alishinda vikombe vingi zaidi akiwa na Arsenal chini ya Wenger.

KOLO TOURE

Tusimsahau mlinzi, Kolo Toure ambaye alikumbwa na matatizo nyakati za mwisho mwisho akiwa na Arsenal.

Kolo alisainiwa na Wenger kwa pauni 150,000 na beki hiyo raia wa Ivory Coast ambaye pia alicheza kama mshambuliaji alikuwa mmoja wa wale waliotegemewa kwenye klabu hiyo.
Toure alicheza na magwiji wengine kama Sol Campbell, William Gallas na pia Philip Senderos.

Alishinda mataji matano akiwa na washika bunduki hao na kuchangia mabao 14 kwa jumla ya mechi 326 alizocheza.

ALEX SONG

Alex Song, alikuwa mmoja wa wachezaji bora zaidi wa Afrika waliosainiwa na Wenger.
Licha ya Song kutofikia kiwango cha watangulizi wake kama Patrick Viera na Gilberto Silva, alitoa mchango mkubwa kwa Arsenal.

Alikuwa ni mchezaji mzuri na hata baada ya kuhamia Portsmouth, aliamua kuelekea huko Barcelona.

Hata hivyo, hakushinda taji lolote akiwa na Arsenal. Alisakata kambumbu ya hali ya juu kwenye mechi 218 akiwa na Wenger.

EMMANUEL ADEBAYOR

Yawezekana Adebayor alimuita Wenger mtu feki, lakini, bado anastahili kumshukuru sana kwa kumkuza tangu alipomsaini kutoka Monaco mwaka 2006.

Adebayor haukuweza kuichezea Arsenal kwa misimu mitatu, lakini, ni mmoja wa wachezaji bora zaidi kuichezea Arsenal wakati wa kipindi cha Wenger.

Raia huyo wa Togo alicheza jumla ya mechi 143 na kufunga mabao 62.(BBC Sports).

MAONI YAKO