UWEKEZAJI ni sekta inayokua kwa kasi sana duniani, ambapo nchi zenye maisha tulivu na amani kama Tanzania ndizo zinazofaidika na baraka hizo.

Uwekezaji wa wageni iwapo utafuata masharti ya kuwawezesha vijana wazalendo kupambana na umasikini unafungua milango ya kupunguza wimbi la ukosefu wa ajira.

Hali hii inatokana na vijana wengi kupatiwa fursa za ajira mbali mbali zinazowawezesha kuimarisha maisha yao.

Katika miaka ya hivi karibuni, wawekezaji wa mataifa ya bara la Asia wamekuwa wakikuza biashara na uchumi si nchini kwao tu lakini pia nchi ambazo wanashirikiana nazo katika uwekezaji.

Zamani Zanzibar ilizowea kupokea wataalamu kutoka China wakiwa na ujuzi wa fani mbali mbali hususan madaktari, na hivyo mawasiliano yalikuwa ni jambo ambalo halikupewa umuhimu mkubwa.

Licha ya kuwa lugha hiyo haijaeneea kwa kasi kiasi cha kupishana na watu tu wakikizungumza lakini kasi ya kufundishwa katika taasisi za elimu ina sehemu katika kuongeza kasi ya kukua kwa lugha hiyo.

Nchi kadhaa kwa mfano, wamekuwa na fursa muhimu sana katika uwekezaji katika sekta mbali mbali. Lakini kabla ya kufika huko uwekezaji wa lugha unafungua milango ya kukuza soko la biashara na utalii kwani watu wengi zaidi

wanaweza kukuza mawasiliano na raia wa mataifa hayo.

Hapa Zanzibar, kichina hakikuwa kikionekana kuwa ni lugha yenye thamani katika ulimwengu wa mawasiliano na biashara na badala yake lugha nyengine mashuhuri zilionekana kuwa na soko kubwa la mawasiliano katika

nyanja za utalii kwa kupokea wageni wa mataifa hayo na biashara.

Kinyume na mtazamo wa sasa, lugha imekuwa ni yenye soko kubwa kiasi cha kuwa hata watu wa kawaida sasa wanakifundisha kuanzia vituo vya binafsi na hata Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar na vyuo vyengine nchini.

Ziara zinazofanywa na maofisa mbali mbali wa Zanzibar nchini China nazo pia zinafungua milango ya kuwavutia wengi zaidi kujifunza lakini pia kuiga baadhi ya tamaduni zao kidogo kidogo ni kuongeza kuitangaza nchi hiyo katika sura ya dunia na utamaduni.

Kama hilo halitoshi uwekezaji katika sekta za uvuvi na bahari kuu zinazotarajiwa kuwekezwa Zanzibar ni hatua nyengine muhimu itakayowezesha kupunguza tatizo la ajira kwa vijana. Hali hii inatokana na upatikanaji wa rasilimali ya bahari inayoaminika kuwa na samaki wa aina mbali mbali.

Hapa panaweza pakatoa njia mbali mbali za uvuvi wa samaki moja kwa moja na hivyo vijana kujiajiri kwa kuvua tu lakini pia shughuli hizo zinaweza kuzalisha sekta nyengine.

Miongoni mwa sekta hizo ni uzalishaji wa viwanda kwa kusindika samaki au kuwahifadhi katika namna nyengine mbali mbali na kuuzwa ama katika soko la ndani au nje ya nchi.

Kufanikiwa kwa miradi kama hiyo kuende sambamba na uhifadhi wa mazingira ya baharini ambayo ni chanzo muhimu cha uzalishaji wa samaki.

Pamoja na hatua hiyo ambayo itazishirikisha sekta za mazingira za serikali na za watu binafsi kuimarisha mazingira ya viumbe wa bahari kuambatane na utoaji

wa elimu kwa jamii katika kutunza mazingira.

Tunasema hivi kwa sababu, tatizo la uharibifu wa mazingira ni tatizo ambalo kwa muda mrefu limelalamikiwa hali ambayo imekuwa ikisababisha hasara kubwa kwa kupoteza mazalio ya samaki.

Miongoni mwao ni ukataji wa mikoko, uvuvi wa kutumia nyavu za macho madogo, kutupa taka katika maeneo ya fukwe na nyenginezo. Juhudi za wasimamizi wa ustawi wa mazingira kusimamia uhifadhi wa mazingira zilizochukuliwa ni lazima zipongezwe lakini uangalizi zaidi unahitajika kupambana na wakaidi wanaoharibu na kuchafua mazingira.

Tunapenda jamii ifahamu kuwa uwekezaji hauwezi kufanikiwa bila ya kuwashirikisha wananchi kwa kuwapa elimu ya manufaa watakayoweza kuyapata katika uwekezaji huo ili na wao kutekeleza wajibu wao kulinda rasilimali ya bahari kuu.

MAONI YAKO