KYLIAN MBAPPE

KYLIAN MBAPPE

MANCHESTER CITY inataka kufanya usajili wa mshambuliaji wa  Paris St-Germain 18  Kylian Mbappe, ikiwa klabu hiyo ya Ligue 1 itashindwa kutimiza masharti ya fedha za mchezaji huyo ambaye yupo kwa mkopo wa muda mrefu klabuni hapo akitokea Monaco mwezi Agosti. (Sunday Mirror)

BRENDAN RODGERS

BOSI wa Celtic  Brendan Rodgers yumo katika orodha ya makocha wanne ambao wanaweza kurithi mikoba ya Antonio Conte wa  Chelsea,  (Sunday Express)

ROBERT LEWANDOWSKI

CHELSEA imevutia na mshambuliaji wa Bayern  Robert Lewandowski 29, huku klabu ya Real Madrid nayo pia ikidaiwa kumtaka mchezaji huyo. (Daily Star Sunday)

HARRY MAGUIRE

MANCHESTER UNITED inafikiria kumsajili beki  kutoka Leicester City  25 Harry Maguir. (Sunday People)

KIERAN TIERNEY

BOSI wa United Jose Mourinho amevutiwa na beki wa Celtic  20 na timu ya taifa ya Scotland  Kieran Tierney. (ESPN)

BOBBY DUNCAN

LIVERPOOL inajipanga kumasaini mshambuliaji wa  England U-17 r Bobby Duncan, ambaye ni binamu wa mchezaji wa zamani wa timu hiyo Steven Gerrard  na mabye alikulia katika Akademi ya  Manchester City .(Sun on Sunday)

MAONI YAKO