NA MADINA ISSA

MKUU wa Mkoa wa Mjini Magharibi, Ayoub Mohammed Mahmoud, amewaagiza maofisa wilaya na mkoa huo, kukutana na bodi ya elimu ya mkoa kila baada ya mwenzi mmoja, badala ya mienzi mitatu ili kuzikabili changamoto za sekta ya elimu katika mkoa huo.

Aliyasema hayo alipokuwa akizungumza na maofisa wilaya za mkoa huo, Mwenyeviti wa kamati za skuli na walimu wakuu katika kikao cha kutathmini elimu, kilichofanyika skuli ya Haileselassie.

Alisema hali hiyo itarahisisha kubaini changamoto zinazoikabili sekta ya elimu na kuzipatia ufumbuzi.

Alisema hali ya elimu katika mkoa huo haipo vizuri kwani matokeo ya mitihani kitaifa ya kila mwaka hayaridhishi ambapo katika matokeo ya kidato cha sita mwaka 2016, skuli saba zilikuwa miongoni mwa skuli 10 Tanzania zilizofanya vibaya.

Aidha alisema mwaka 2017 kwa matokeo ya kidato cha nne, skuli mbili za mkoa huo zimo katika kundi la skuli 10 za mwisho kitaifa.

MAONI YAKO