LONDON, ENGLAND

ASRENAL jana imezidi kufanya vibaya baada ya kupoteza mchezo wake wa Ligi Kuu England dhidi ya Newcastle United, pambano ambalo li;likuwa gumu na la kupendeza kwa muda wote.

Kwa matokeo hayo Newcastle imefikisha pointi 41 na kupanda hadi nafasi ya 10, huku Arsenal ikiendelea kusota na pointi zake 54 ikiwa nafasi ya sita, na matokeo hayo yanaendeleza rikodi mbaya ya  Arsenal kwa Newcastle.

Arsenal, ambayo ilitinga hatua ya nusu fainali ya  ligi ya  Europa League kwa kuitoa  CSKA Moscow ya Urusi Alkhamis iliyopita.

Pierre-Emerick  na Aubameyang pamoja na Alexandre Lacazette, walicheza pamoja kwa mara ya kwanza .

 Arsenal ilikuwa ya kwanza kupata bao lililofungwa na AlexandreLacazette  ndani ya dakika ya 14, bao ambalo liliwachonga ukali Newcastle, ambao walisawazisha dakika ya 29 kupitia kwa   Pérez, mabao ambayo yalidumu hadi kipindi cha kwanza kinamalizika.

 Kipindi cha kilianza kwa Newcastle kupanga mashambulizi kusaka bao la pili juhudi ambazo zilizaa matunda dakika ya 68 lililofungwa na Ritchie.

MAONI YAKO