N’GOLO KANTE
KIUNGO wa kati wa Chelsea na Ufaransa, N’Golo Kante (26), ni miongoni mwa wachezaji ambao Paris St-Germain inapanga kujaribu kuwanunua mwishoni mwa msimu. (Canal via Goal.com).

TIMO WERNER
MSHAMBULIAJI Mjerumani wa RB Leipzig, Timo Werner (22), amewaambia Liverpool na Manchester United wasiwe na matumaini ya kumchukua mwishoni mwa msimu. (Mirror).

ANTOINE GRIEZMANN
MSHAMBULIAJI wa Atletico Madrid, Antoine Griezmann (26), naye anadaiwa kuanza kutafuta nyumba eneo la Catalonia katika kinachoaminika kwamba ni maandalizi yake akitarajia uwezekano wake wa kuhamia Barcelona. (Marca).

DIEGO SIMEONE
MENEJA wa Atletico Madrid, Diego Simeone, amepuuzilia mbali uvumi kuhusu uwezekano wa Mfaransa Antoine Griezmann kuhama hivi karibuni. (Goal.com).

EMRE CAN
JUVENTUS wapo tayari kutoamua kuhusu kiungo wa kati wa Liverpool, Emre Can hadi mwisho wa msimu. Mjerumani huyo mwenye umri wa miaka 24, atamaliza kutumikia mkataba wake wa sasa Anfield Julai na anaweza kujiunga na miamba hao wa Italia bila ya ada yoyote wakati huo. (Liverpool Echo).

ALBAN LAFONT
ARSENAL wanakabiliwa na ushindani kutoka kwa Napoli na Roma katika juhudi zao za kutaka saini ya kipa Mfaransa, Alban Lafont mwenye umri wa miaka 19 ambaye anaichezea Toulouse. (L’Equipe).

ALAN PARDEW
MENEJA wa West Brom, Alan Pardew, alitarajiwa kufanya mazungumzo na wamiliki wa klabu hiyo jana kuamua iwapo ataendelea kusalia kazini. (Guardian).

MARK NOBLE
NAHODHA wa West Ham, Mark Noble huenda asiadhibiwe hata baada yake kuonekana akikabiliana na shabiki aliyekuwa ameingia uwanjani wakati wa mechi. (Mail)

RONY LOPEZ
MRENO anayechezea Monaco, Rony Lopes (22), amesema, angelipenda kurejea Manchester City siku za usoni. Aliihama klabu hiyo 2015. (Manchester Evening News).

CHRIS COLEMAN
MENEJA wa Sunderland, Chris Coleman, amesema, alilazimika kubahatisha kuhusu wachezaji walionunuliwa na klabu hiyo mwezi Januari baada ya klabu hiyo kuendelea kutatizika hata baada yao kuwasili ‘Stadium of Light’. (Sunderland Echo).

ALEKSANDAR MITROVIC
MENEJA wa Newcastle, Rafael Benitez, atatathmini upya mustakabali wa mshambuliaji wa Serbia Aleksandar Mitrovic katika klabu hiyo mwezi Mei. Hii ni baada ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23 kung’ara akiwa kwa mkopo katika klabu ya Fulham inayocheza ligi ya ‘Championship’. (Newcastle Chronicle).

MAONI YAKO