NA MASANJA MABULA, PEMBA

JUMLA ya kete 688 za unga unaodhaniwa kuwa ni dawa za kulevya aina hereoine, zimekamatwa na jeshi la polisi mkoa wa kaskazini Pemba, kufuatia operesheni iliyofanywa na jeshi hilo.

Akithibitisha hilo, Kamanda wa polisi mkoa huo, Haji Khamis Haji, alisema wamemkamata kijana Shibu Ali Juma (35) mkaazi wa Limbani Wete akiwa na dawa hizo.

Alisema mtuhumiwa alikatwa ndani ya nyumba yake na baada ya kufanyiwa upekuzi alipatikana akiwa na kete 688 za unga unaodhaniwa kuwa ni dawa za kulevya.

Alisema kwa sasa mtuhumiwa anaendelea kuhojiwa na upelelezi ukikamilika atafaikishwa mahakamani kujibu tuhuma zinazomkabili.

Aliwaomba wananchi kuendelea kushirikiana na jeshi la polisi kwa kutoa taarifa sahihi ambazo zitafanikisha kuwakamata wanaojihusisha na biashara ya dawa za kulevya.

“Tunawashukuru sana wananchi waliofanikisha kutupatia taarifa hizi, nawaomba waendelea kutupa ushirikiano ili tuweze kufanikisha mapambano dhidi ya madawa ya kulevya,” alisema.

MAONI YAKO