NA MWANDISHI WETU

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein, amefanya uteuzi wa viongozi katika taasisi mbali mbali za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Walioteuliwa ni Abdulla Hassan Mitawi kuwa Naibu Katibu Mkuu katika Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais.

Wengine ni Saum Ali Said alieteuliwa kuwa Mkurugenzi Mipango, Sera na Utafiti katika Wizara ya Vijana, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Joseph John Kilangi, alieteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Idara ya Uendeshaji na Utumishi katika wizara hiyo.

Kwa mujibu wa taarifa kwa vyombo vya habari iliyosainiwa na Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi, Dk. Abdulhamid Yahya Mzee, uteuzi huo umeanza Machi 12, 2018.

MAONI YAKO