BARCELONA,Hispania

KIUNGO mshambuliaji wa Barcelona, Ivan Rakitic, amesema milango ipo wazi kwa Neymar kurejea Nou Camp.

Neymar aliondoka Barcelona kwenda PSG ya Ufaransa kwa ada ya uhamisho wa pauni milioni 198, mwezi Agosti mwaka 2017.

Rakitic, amesema, ukiachilia mbali uhusiano wao na urafiki, anamkaribisha mshambuliaji huyo kutokana na aina ya uchezaji alionao pia angelipenda kuona akiwa katika kikosi cha kwanza.

Kumezuka taarifa za Neymar kutaka kurudi Barcelona, ikielezwa ni kutokana na kutofanya vizuri kwa PSG kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Kwa mujibu wa gazeti la Mundo Deportivo, Mbrazil huyo anajutia kuondoka Barcelona na taarifa zinasema anataka kurejea klabuni hapo mwaka 2019.

Lakini pia inaelezwa Paris St-Germain wapo wazi katika kumuuza mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 26, kwa klabu yake ya zamani ya Barcelona au kwa washindani wao, Real Madrid.

Neymar anataka kuondoka Paris Saint-Germain kwa ajili ya timu ya ushindani zaidi, lakini, miamba hiyo ya ‘Ligue 1’ hawana nia ya kumruhusu Brazil huyo kuondoka Parc des Princes msimu huu, kwa mujibu wa mtaalamu wa soka wa Sky Sports, Guillem Balague.

Neymar ambaye kwa sasa anauguza majeraha baada ya kuumia wakati wa pambano dhidi ya Marseille mwanzoni mwa Machi, amesaini mkataba wa miaka mitano na klabu hiyo ya jijini Paris.

Hata hivyo, pamoja na kufunga mabao 29 na kusaidia 19 katika mechi 30 kwenye mashindano yote katika msimu wake wa kwanza, lakini, ujio wake PSG hakukuzuia klabu hiyo kuondolewa kutoka Ligi ya Mabingwa Ulaya kwenye hatua ya 16 bora na Real Madrid wiki hii.

“Tutaendelea kusikia katika miezi michache ijayo, hata msimu ujao, akionyesha Neymar anataka kuondoka PSG, kutoka pembe tofauti”, Balague aliiambia Sky Sports.

“Ninatarajia ni kutoka chanzo sawa, mshiriki wake.Nadhani yeye alitambua PSG sio mahali pake, nadhani anataka kuangalia pahali pa ushindani zaidi pa kucheza.”

Mabingwa wa La Liga na Ulaya, Madrid wanaripitiwa kuangalia kumrejesha Neymar Hispania tena msimu ujao, ingawa PSG haitaki kuidhinisha kuondoka kwa mchezaji, amesema Balague.(Sky Sports).

MAONI YAKO