NA NASRA MANZI

CHAMA cha soka (ZFA) Wilaya ya Kusini kimetakiwa kushirikiana na klabu kuondosha changamoto, zinazozikabili timu za wilaya hiyo kwa lengo la kukuza soka na kufikia malengo.

Akizungumza na Zanzibar leo Mjumbe wa Baraza la Michezo Wilaya hiyo Mussa Kinole huko Makunduchi,alisema vyema chama hicho kikakaa na klabu hizo, kama sehemu ya ni hatua ya kujitathmini juu ya utendaji wake wa kazi.

Alisema ni bora viongozi kuwa na utaratibu wa kuziita klabu na kufahamu changamoto ambazo zinawakabili, kwa lengo la kiufanya ligi ya wilaya hiyo kuwa bora zaidi.

Alisema kuwa hivi sasa Wilaya ya Kusini kwa muda mrefu imekosa mvuto na hamasa kutokana na umaskini unaozikabili klabu hizo.

Kinole alisema ukosefu wa vifaa vya michezo huwafanya viongozi kuchangishana, jambo ambalo kwa kiasi kikubwa huchangia kuzidi kuporomoka kwa soka.

Hata hivyo alisema Wilaya hiyo imekuwa na michezo mingi na vipaji lakini tatizo kubwa ni usimamizi wake, hautiliwi mkazo kwa viongozi husika.

Alisema ni ukweli kuwa kiwango cha mpira kwa upande wa Wilaya kimeshuka na jitihada za makusudi zinahitajika kuchukuliwa, katika kurejesha hadhi ya soka wilayani humo.

Alisema umoja na mashirikiano utapelekea kupatikana kwa maendeleo na kujiepusha na chuki zisizo msingi, ambazo zinachangia kwa kiasi kikubwa kudumaza soka.

MAONI YAKO