MRATIBU Idara ya Michezo na Utamaduni Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Pemba, Mzee Ali Abdalla (kulia), akimkabidhi vifaa vya michezo mmoja wa walimu wa skuli Kisiwani Pemba, ikiwa ni utekelezaji wa mradi wa 'Sport 55'(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA).

NA ABDI SULEIMAN, PEMBA

WALIMU wa michezo kutoka skuli 30 zilizokabidhiwa vifaa vya michezo kupitia mpango wa ‘Sport 55’, wametakiwa kuvitunza na kuvithamini vifaa hivyo, pamoja na kuvitumia kwa kuwafundishia wanafunzi na sio kwa klabu vyengine.

Akikabidhi vifaa hivyo kwa walimu wa michezo, Mratibu wa Idara ya Michezo na Utamaduni Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Pemba Mzee Ali Abdalla, alisema vifaa hivyo vimetolewa kwa ajili ya skuli na sio kwenda kufundishwa katika klabu za mitaani.

“Lengo ni kukabidhi vifaa ili kwenda kutekeleza mpango kazi kwa vitendo, huu ni mpango wa miaka miwili skuli za sekondari na msingi kwa wilaya nne za Pemba, lakini kuna skuli nyingine tumeziongeza na kufikia 30” alisema.

Wakizungumza baada ya kukabidhiwa vifaa hivyo baadhi ya walimu wa michezo kisiwani Pemba, wameahidi kuvitumia kwa lengo lililokusudiwa.

Mwalim Salma Ali Suleiman kutoka skuli ya Mitiulaya, alisema vifaa vitasaidia sana kuendeleza michezo katika skuli hiyo, kwani watoto wataweza kucheza michezo mbali mbali.

MAONI YAKO