PARIS, Ufaransa

USHINDI mara mbili katika mechi za mchezaji mmoja mmoja aliopata Venus Williams kwenye mchuano wa hatua ya robo fainali ya kimataifa kati ya Marekani na Uholanzi, umeisaidia timu ya taifa ya Marekani kufuzu hatua ya nusu fainali.

Venus aliwashinda Richel Hogenkamp na Arantxa Rus kwa mechi mfuatano zilizokuwa na matokeo ya yenye alama 7-5, 6-1 na 6-1, 6-4.
Ushindi mwengine muhimu wa Marekani ulitokana na matokeo ya ushindi wa CoCo Vandeweghe aliyemfunga, Richel Hogenkamp kwa 4-6, 7-6, 6-3.

Katika mechi za wachezaji wawili wawili, Serena aliungana na dada yake Venus kuunda timu moja na lakini walipoteza kutokana na Serena kutokuwa imara bado.
Lakini kwa kufuzu hatua ya nusu fainali, mwezi Aprili Marekani watacheza na Ufaransa ambao nao wamefuzu baada ya kuishinda timu ya taifa ya Ubeligiji.(AFP)

MAONI YAKO