LONDON, England

MENEJA wa Manchester United, Jose Mourinho, amesema, klabu yake haingelifunga bao hata kama ingelicheza kwa saa 10 kufuatia kikosi hicho kupoteza 1-0 dhidi ya Newcastle.
Goli la dakika ya 65 la Matt Ritchie lilisababisha mashetani wekundu hao kushindwa kwa mara ya tano msimu huu.

Sasa Manchestrer United wapo nyuma ya vinara Manchester City kwa pointi 16.
“Miungu yao ya soka ilikuwa wazi nao”, aliseam Mourinho. “Haingewezekana leo (juzi).”
Meneja huyo wa zamani wa Chelsea alisema, Newcastle walicheza kama wanyama kushinda nyumbani kwa mara ya kwanza tangu Oktoba.

“Hisia zangu ni kuwa tungelicheza kwa saa 10 na hatungelifuga bao”, alisema.
“Tulikuwa na fursa wakati tulipokuwa 0-0, alisema Mourinho, Alexis Sanchez alikuwa na fursa ya kufunga na kisha fursa nyengine dakika za 20 na 25 za mwisho”
Mpira wa adhabu ndogo ambao ulichangia bao la Ritchie, ilipatikana wakati beki wa United, Chris Smalling, alipolaumiwa kwa kuruka.(BBC Sports).

MAONI YAKO