NA ABDI SULEIMAN, PEMBA

TIMU ya Opec imefanikiwa kurudi kileleni mwa ligi kuu ya Zanzibar kanda ya Pemba , baada ya kuitandika timu ya Chuo Basra bao 1-0, mchezo uliopigwa katika uwanja wa Gombani.

Timu hizo zilikiana zakipindi cha kwanza kwa kasi kubwa, huku kila timu ikicheza kwa umakini mkubwa.

Bao pekee la washindi lilifungwa na Moris Rauli Katumbo katika dakika ya 15 ambalo  limeifikisha Opec kuwa na pointi  28 na kuishusha Mwenge.

Timu ambazo hadi sasa ziko katika mstari mwekundu ni Chuo Basra, Okapi, Younger Islander, FSC, Chipukizi na Wawi Star.

MAONI YAKO