CAIRO, MISRI

MKUTANO  wa dharura wa mawaziri wa mambo ya nje wa Umoja wa nchi za Kiarabu, Arab League, umefanyika mjini Cairo, Misri, ambapo wajumbe wameukosoa vikali uamuzi wa Rais Donald Trump wa Marekani kuitambua Jerusalem kama mji mkuu wa Israel.

Wameitaka Marekani kuachana na mpango wake, kwani utaongeza ghasia katika ukanda huo.

Katibu Mkuu wa umoja huo, Ahmed Aboul Gheit, amezitolea wito nchi zote duniani zinazopenda amani kupaza sauti zao kwa uwazi na kuukataa uamuzi huo wa Trump usio halali. Pia amezitaka nchi hizo kulitambua taifa la Palestina, huku Jerusalem Mashariki ukiwa mji mkuu wake.

Mkutano huo uliofanyika jana na kuwakutanisha pamoja mawaziri wa mambo ya nje wa nchi wanachama, unafanyika wakati ambapo maandamano yakiendelea kwa siku ya tatu mfululizo katika Ukingo wa Magharibi na Ukanda wa Gaza.

Mkutano huo uliofanyika kwa muda wa saa mbili na nusu, ulimalizika baada ya kiasi ya wajumbe wakuu 20 kuzungumza.DW

MAONI YAKO