OLIVIER GIROUD

MSHAMBULIAJI wa Arsenal  Olivier Giroud anataka kutolewa kwa mkopo ili kupata nafasi ya kucheza timu ya taifa ya Ufaransa kwenye kombe la dunia.West Ham na Crystal Palace zote zinavutiwa na mchezaji huyo 31. (Sunday Mirror)

EDEN HAZARD

MSHAMBULIAJI wa Chelsea  Eden Hazard 26, amesema hana mpango wa kuhama klabuni hapo, licha ya kuwepo uvumi wa kuhamia  Real Madrid. (Onze Mondial, via Sun on Sunday).

JOE HART

KIPA Joe Hart 30 hayupo tayari kumaliza kucheza kwa mkopo na kuondoka  West Ham mwezi Januari. (Sunday Times – subscription required).

PHILIPP MAX

KLABU za Liverpool,Manchester United na  Tottenham zimeungana na Everton, kumuwania beki wa kushoto wa  Augsburg Philipp Max, 24. (Mail on Sunday).

JOSH EPPIAH

EVERTON na West Ham zinamfuatilia kwa karinbu mshambuliaji wa Leicester Josh Eppiah, 19. (ESPN)

ALPHONSO DAVIES

MANCHESTER UNITED imempa nafasi winga 17 Alphonso Davies, kutoka klabu ya  MLS side Vancouver Whitecaps, kufanya majaribio klabuni hapo . (CTV, via Sunday Express)

HATEM BEN ARFA

WACHEZAJI wa Paris St-Germain mshambuliaji Hatem Ben Arfa, 30 na winga  Lucas Moura 25,wamezungumzia juu ya uhamisho wao ifikapo mwezi  Januari . (ESPN)

KAMIL GRABARA

MLINDA mlango wa Liverpool  Simon Mignolet amemtumia meseji  Kamil Grabara kwa kumpongeza baada ya mchezaji huyo  18 kusaini mkataba mpya  (Sunday Express)

MAONI YAKO