NAIROBI, KENYA

MWANAFUNZI wa Chuo Kikuu wa mwaka wa tatu ameuawa na mpezi wake wa kiume kwa shutuma za kutokuwa mwaminifu.

Tukio hilo lilitokea majira ya asubuhi ya Jumamosi katika nyumba ya kulala wageni katika mji mdogo wa Bondo.

Valerie Apondi,23, ambaye alikuwa kisomea Shahada ya kwanza ya uchumi katika Chuo kikuu cha Jaramogi Oginga Odinga cha Sayansi na Teknolojia , alikutwa akiwa amefariki na kuenea damu katika chumba ambacho walikodi.

Mhudumu wa nyumba hiyo ya kulala wageni  Benson Onchiri alisema, wawili hao walokodi chumba hixho Ijumaa majira ya saa mbili usiku.

Mtuhumiwa  Collins Oluoch Ogweno, 25, ambaye ni muuguzi katika hospitali ya  Nightingale iliopo Kisumu anadaiwa kumuua Apondi kwa kutumia panga.

Rafiki wa karibu wa marehemu ambaye ahakutaka jina lake litajwe alisema,  Oluoch alimshawishi Valerie kuondoka chuoni ingawa hakutaka kufanya hivyo.

“Apondi hakuwa akitaka kwenda pahala popote na  Oluoch lakini baada ya dakika chache akakubali na wakatoka pamoja kuelekea Bondo,” alisema.

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo, Kaimu Kamanda wa Polisi mjini Bondo, Robert Makau alisema walikuta panga na maji yaliyosadikiwa kuwa ni sumu katika eneo la tukio.

Makau alisema kwamba hiyo si mara ya kwanza kwa wawili hao kuwa na mzozo.

Aidha ilielezwa kwamba wawili hao pia walikuwa tayari wameshapata mtoto mmoja.

Hata hivyo, mwili wa marehemu ulipelekwa katika chumba cha kuhifadhia maiti katika hospitali ya Bondo wakati upelelezi ukiendelea . THE STAR

MAONI YAKO