Lionel Messi

LIONEL MESSI
LIONEL Messi alikataa ofa ya pauni 850,000 kwa wiki kutoka Manchester City kabla ya kusaini mkataba mpya na Barcelona. (Marca).

JURGEN KLOPP
MENEJA wa Liverpool, Jurgen Klopp, amesema, hana uhakika ikiwa mchezaji wa kiungo cha kati, Philippe Coutinho bado atakuwa Anfield baada ya mwezi Januari. Barcelona ilitoa ofa mara tatu kwa raia huyo wa Brazil msimu huu. (Daily Star).

PEP GUARDIOLA
MENEJA wa Manchester City, Pep Guardiola, atarudi na ofa kubwa ya kumsaini mshambuliaji wa Arsenal na Chile Alexis Sanchez (28), mwezi Januari. (Independent).

THEO WALCOTT
KLABU ya Everton wamewaulizia Arsenal kuhusu mshambuliaji Theo Walcott (28), ambaye bado hajaanza kucheza msimu huu. (Daily Mail).

ALEX SANDRO
CHELSEA wamepewa matumaini baada ya taarifa kuwa mlinzi wa Brazil, Alex Sandro (26), anataka kuhama Juventus. (Telegraph).

WILLIAM CARVALHO
WEST Ham wataanza tena kumuwinda mchezaji wa kiungo cha kati wa Sporting Lisbon, William Carvalho (25). (Sun).

IVAN PERISIC
KIUNGO wa Manchester United,Ivan Perisic (28), amefichua kuwa kocha wa Inter Milan, Luciano Spalletti alijaribu kumshawishi asihame Italia baada ya kuhamia Old Trafford. (Mediaset via Manchester Evening News).

SERGEJ-MILINKOVIC SAVIC
KLABU ya Manchester United waliwatuma maajenti kumtazama mchezaji wa kiungo cha kati wa Lazio, Sergej-Milinkovic Savic (22), wakati wa ushindi wa 2-1 dhidi ya Sampdoria wiki iliyopita. (Sun).

JACK HENDRY
KLABU za Southampton, Newcastle United na Crystal Palace wanammezea mate mlinzi wa Dandee, Jack Hendry (22). (Daily Mail).

FYODOR SMOLOV
WEST Ham watakabiliwa na ushindani kutoka Real Madrid kusaini, Fyodor Smolov (27), mshambuliaji wa Krasnodar na Urusi. (Daily Mail).

Aleksandar Mitrovic

ALEKSANDAR MITROVIC
MSHAMBULIAJI wa Newcastle, Aleksandar Mitrovic (23), anaweza kurejea Anderlecht mwezi Januari huku akiendelea kuchanganyikiwa klabu hapo. (Nieuws Blad via Chronicle).

MAONI YAKO