NA ASYA HASSAN

MTU mmoja anashikiliwa na polisi Mkoa wa Kusini Unguja kwa tuhuma za kuwabaka watoto wannen wenye umri wa kuanzia miaka minane hadi 12.

Mtuhumiwa huyo ametambulika kwa jina la Othman Ali Simai (Fundi Achu) mwenye umri wa miaka 30, mkaazi wa Mtarika Muyuni ‘A’ wilaya ya kusini Unguja.

Kamanda wa Polisi mkoa huo, Makarani Khamis, alisema awali mtuhumiwa  alidaiwa kuwabaka watoto saba lakini baada ya kufikishwa hospitali kwa kuchunguzwa wanne ndio waliobainika kubakwa na watatu walikutwa wako salama.

Alisema watoto wawili kati yao ni ndugu wa familia moja, huku wawili wengine wakiwa ni watoto wa baba mkubwa na mdogo.

Alisema polisi wanaendelea kumshikilia mtuhumiwa kwa  upelelezi na ukikamilika atafikishwa katika vyombo vya sheria.

Alitumia fursa hiyo kuiomba jamii kutokwa mbali na  watoto wao kutokana na matukio ya udhalilishaji  kuongezeka siku hadi siku.

Baadhi ya wazazi ambao watoto wao wamefanyiwa vitendo hivyo waliiomba  serikali kumchukua hatua kali mtuhumiwa ikiwemo kumpatia kifungo cha maisha jela.

Mmoja ya mzazi, alisema alimtuma mwanawe akatafute makuti aliporudi alibaini anatoa harufu ndipo alipoingiwa na hofu na kuaza kumuhoji na kumchapa.

Alisema limtaja mtuhumiwa huyo kuwa ndie aliemfanyia kitendo hicho na kuwataja wenzake wengine waliofanyiwa ukatili huo.

Alisema waliwapeleka watoto hao hospitali ya Makunduchi kwa uchunguzi ndipo ilipobainika watoto wanne wamefanyiwa udhalilishaji.

Sheha wa shehia ya Muyuni ‘A’, Maulid Hassan Zidi, alithibitisha kutokea tukio

MAONI YAKO