KAMPALA, UGANDA

JAJI wa Uganda amechaguliwa kuungana na Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu  (ICC)  ya The Hague, iliopo  Netherlands.

Baraza la mataifa wanachama lililokaa mjini  New York Jumanne , lilimchagua Jaji  Solome Bossa, ambaye ni Jaji wa Mahakama ya Rufaa Uganda, baada ya mzunguko wa nne wa kura.

Balozi  Adonia Ayebare, Mwakilishi Mkaazi wa Uganda kwa Umoja wa Mataifa , alisema walifanyakazi kubwa ili kuhakikisha anachaguliwa.

ICC iliundwa kwa sheria ya  2002 ya Rome  ili kujaribu kesi za mauaji ya halaiki, jinai za kivita na jinai dhidi ya ukiukaji wa haki za binadamu.

Ayebare alisema Afrika, iliwakilisha wagombea wanne na ambapo majaji wengine waliochaguliwa walitokea nchi za  Benin, Japan na  Peru.

Kuchaguliwa kwa Jaji  Bossa, kwa mujibu wa  Ayebare, ni jambo muhimu sana kwa kuwa  ICC ni mahakama ya kudumu Ulimwenguni katika kushughulikia kesi za maujai  ya halaiki, jinai za kivita na jinai za ukiukaji wa haki za binadamu.

“Ushindi huu ni kura ya kujivunia kwa Mahakama za Uganda na Ubalozi katika Umoja wa Mataifa,” alisema.

Uganda ilimchagua Jaji  Bossa, ambaye kazi zake za kisheria zilidumu kwa miongo mitatu, kwa kuwa  “Jaji mwenye uadilifu wa hali ya juu katika taifa , kikanda na ngazi ya Kimataifa,” kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kupitia mtandao wa Majaji.

Waangalizi wa masuala ya kisheria watakuwa na hamu kubwa ya kutazama utendaji wa Jaji  Bossa akiwa  The Hague ikizingatiwa kwamba Rais  Yoweri Museveni awali alielezea mashaka ya mamlaka na mwenendo wa ICC.

Hata hivyo alibadili kauli hiyo baada ya  ICC kuanza kumsaka kiongozi wa  LRA ,  Joseph Kony  na jinai nyengine za kivita nchini  Uganda. DAILY NATION

MAONI YAKO