Aliwahi kuwa Spika wa Singapore

HALIMAH binti Yacob amezaliwa Ogasti 23, 1954 nchini Singapore, kwa sasa ni mwanasiasa na hii ni baada ya kushinda urais wiki iliyopita. Halima anakuwa mwanamke wa mwanzo nchini Singapore kuwa rais baada ya kutanguliwa na marais saba na yeye akiwa wa nane.

Chama chake ni cha People’s Action Party (PAP), pia Halima aliwahi kuwa spika wa Bunge la Singapore kuanzia Januari 2013 hadi Ogasti 2017.

Aidha aliwahi kuwa mbunge akiwakilisha kundi maalumu kati ya mwaka 2001 hadi 2015.

Mnamo Ogasti 7 mwezi uliopita Halimah alijiuzulu nafasi zote za uspika na ubunge ambapo chama chake cha PAP, kilimteua kugombea urais wa Singapore ambao ulifanyika kama wiki mbili zilizopita.

Septemba 13 Halimah alitangazwa kuwa ni Rais wa Singapore baada ya kushinda uchaguzi na hivyo kuandika historia ya kuwa rais wa kwanza mwanamke nchini humo.

Aliapishwa siku iliyofuata ambapo hivi sasa tayari ameanza kutekeleza majukumu yake katika ikulu ya rais.

Baba yake Halimah alikuwa ni mlinzi ambae alifariki wakati Halimah akiwa ni binti wa miaka minane na tangu wakati huo Halimah aliishi na mama yake.

Ameanza elimu yake katika skuli ya Tanjong Katong Girls’ School, ambapo baadae alipata elimu ya juu katika chuo kikuu cha Taifa cha National University of Singapore ya shahada ya kwanza ya sheria  mwaka 1978.

Pia alikamisha mafunzo yake ya shahada ya pili ya sheria katika chuo kikuu cha National University of Singapore na baadae kuhitimu elimu ya ngazi ya daktari wa  sheria Julai 2016.

Halimah alianza kazi kama ofisa wa sheria katika muungano wa vyama vya biashara vya taifa.

Na baadae alikuwa ni mkurugenzi wa Idara ya huduma za sheria hiyo ilikuwa ni mwaka 1992.

Aidha aliteuliwa mkurugenzi mkuu wa taasisi ya huduma za maktaba ambayo kwa sasa inajulikana kama taasisi ya mafunzo ya maktaba ya chuo cha Ong Teng Cheong mwaka 1999.

KISIASA

Halimah alianza siasa rasmi mwaka 2001ambapo alichaguliwa kuwa mbunge akiwakilisha kundi la  ‘Jurong’ nafasi maalumu.

Nafasi hiyo aliendelea nayo hadi uchaguzi mkuu wa mwaka 2011 ambapo Halimah aliteuliwa waziri katika ofisi ya rais anaishughulikia uchumi.

Baadae alikuwa waziri wa nchi katika ofisi ya rais anaeshughulikia ustawi wa jamii na maendeleo ya familia.

Pia aliwahi kuwa mwenyekiti wa jiji la Jurong hadi Januari 2015 ambapo alikuwa ni katibu mkuu wa kamati tendaji ya bodi ya maamuzi ya juu ya chama cha PAP.

Katika uchaguzi mkuu wa mwaka , Halimah alikuwa katika kundi maalumu kwa ajili ya kampeni.

NAFASI YAKE YA USPIKA

Mnamo Januari 8, 2013,Waziri mkuu wa Singapore, Lee Hsien Loong, alimteua  Halimah Yacob kuwa Spika wa Singapore na hiyo ilitokana na kustaafu kwa aliekuwa spika, Michael Palmer.

Alianza rasmi majukumu yake Januari 14, 2013 na kuwa mwanamke wa mwanzo ya kihistoria kukamata nafasi kama hiyo ya juu nchini Singapore.

MUUNGANO WA KIBIASHARA

Halimah alianza shughuli za kibiashara na kupelekea kuanzisha muungano wa vyama vya taifa vya biashara ambapo alikuwa kama msaidizi katibu mkuu wa muungano wa biashara.

Aidha alikuwa ni katibu mtendaji wa muungano wa wafanyakazi viwanda na mambo mengine yanayohusiana na shughuli za umeme.

Halimah pia aliteuliwa msaidizi mwenyekiti wa mkutano wa kamati ya  mkutano wa kimataifa wa vyama vya wafanyakazi mjini Geneva kuanzia mwaka 2000 hadi 2002 na 2005.

Hata hivyo mwaka 2003 hadi 2004, alishika wadhifa wa kuwa msemaji wa kamati ya wafanyakazi wa kamati ya mikutano ya kimataifa kama maendeleo ya rasilimali watu na mafunzo.

KUCHAGULIWA KUWA RAIS

Mnamo Ogasti 6  mwaka huu wa 2017, Halimah alitangaza kujiuzulu nafasi ya uspika na mbunge siku chache kabla ya kuteuliwa kuwa Rais wa Singapore.

Kuteuliwa kwake kunatokana ni lazima kutoka katika jamii ya Malay nchini Singapore ambayo ni kubwa zaidi.

Aidha mnamo Ogasti 25  mwaka 2017, Halimah alizindua kampeni zake rasmi katika mitandao ya kijamii ka website, ikiwa ni pamoja na kuweka mabango ya kumuonesha kugombea nafasi hiyo.

Akiwa na chama chake cha PAP yeye binafsi alikuwa huru kwenye kampeni hizo za uchaguzi.

MAISHA YAKE BINAFSI

Halima akiwa na Mumewe

Halimah ameolewa na mume wake ni Mohammed Abdullah Alhabshee, ambae kwa sasa ameshastaafu, amezaa watoto watano, Halimah ni Muislamu, alikuwa akiishi katika nyumba za umma za taifa huko Yishun.

Makala hii imetayarishwa na HUSNA MOHAMMED kwa msaada wa mtandao.

SHARE
Habari Zilizopita
Habari NyengineUdaku katika Soka

MAONI YAKO